Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2017

MAUAJI KIBITI

SPIKA NDUGAI APOKEA MAUAJI YA KIBITI. Dodoma. Spika wa Bunge Job Ndugai amepokea taarifa ya Kamati ya Ulinzi, Mambo ya Nje na Usalama kuhusu uchunguzi wa tukio la mauaji ya askari polisi wanane yaliyofanywa na watu wasiojulikana katika Wilaya ya Kibiti Aprili 13, mwaka huu. Kamati hiyo ilipewa jukumu hilo na Spika kufuatia mwongozo uliombwa na Mbunge wa Bukombe (CCM),Dotto Biteko  Aprili 18, mwaka huu akitaka Bunge lijadili suala hilo, lakini Ndugai aliamua suala hilo lifanyiwe kazi na kamati na kuwasilisha taarifa kwake. Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amelieza Bunge leo Alhamisi kuwa kamati hiyo ilikutana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwiguli Nchemba na kukusanya taarifa za kina kasha kuandaa taarifa  ambayo imewasilishwa na Spika, naye akaiwasilisha serikalini kwa utekelezaji.

UNENE

YAJUE MADHARA YA UNENE KUPITA KIASI. Imeelezwa kuwa unene uliopitiliza unasababisha vifo vya mapema zaidi ya vifo vinavyosababishwa na kuvuta sigara, kwa mujibu wa utafiti mpya. Watafiti kutoka Cleveland Clinic na New York University School of Medicine waliainisha sababu za vifo nchini Marekani wakitumia takwimu za mwaka 2014 na kubaini kuwa unene kupita kiasi ulisababisha vifo kwa 47% zaidi ya tumbaku. Wakilinganisha data na juhudi za afya ya jamii, watafiti hao walisema tumbaku ingeweza kuongoza list kama isingeweza kuwekewa ukomo wa matumizi ya sigara duniani na kusisitiza kampeni kama hiyo ifanywe pia kupunguza vifo vitokanavyo na unene uliopitiliza. Dr Glen Taksler, Mtafiti wa masuala ya Dawa kutoka Cleveland Clinic na kiongozi wa watafiti hao alisema: “Matokeo haya yanaendelea kuainisha umuhimu wa kupunguza uzito, kujikinga na kisukari na kula kwa kuzingatia afya.”  Matokeo hayo pia yaliainisha umuhimu wa kuhudhuria vituo vya afya na kuzingatia vipaumbele ...